Mwanamume mmoja alitumia udanganyifu na kujidai kuwa mgonjwa
mahututi kwa miaka miwili nchini Uingereza.
Alan Knight, mwenye umri wa miaka 47, kutoka mtaa wa
Swansea, alimuibia mzee mmoja jirani yake pauni elfu arobaini kwa njia ya
udanganyifu na kudai kuwa hengeweza kutembea kutokana na kupooza kutoka
shingoni hadi miguuni.
Hii ilikuwa njama yake ili asiweze kukamatwa kwa kosa hilo.
Inaarifiwa laikwepa polisi mara mbili kwani wakati hupo yeye mwenyewe alijipeleka
hospitani ili asikamatwe na kushitakiwa.
Kila wakati polisin walipotaka kumfikisha mahakamani ,
Knight alijipeleka hospitalini akidai kuwa hali yake imekuwa mbaya zaidi.
Hata hivyo siku zake za mwizi kushikwa zilifika pale wauguzi
walipompata katika chumba chake hospitalini akiwa anakula , kupanguza mdomo
wake na hata kuandika.
Kwa miaka miwili, Night alikwepa mkono wa sheria kwa kudai
kuwa alikuwa hawezi kuamka wala kutembea na pia alikuwa tayari na uraibu wa
kutumia gesi ya oxygen kama mtu ambaye hawezi kupumua bila usaidizi wa gesi
hiyo.
Yote hayo yalikuwa ongo na ambayo yangewezekana tu kwa
sinema.
Alan Knight katika duka la Tesco, alinaswa na polisi kwa
camera ya CCTV akisukuma gari la kubebea bidhaa ndani ya duka hilo wakati
akidai kuwa mgonjwa mahututi.
Afisaa mmoja wa polisi Paul Harry,kutoka South Wales
alisema: ‘Katika kazi yangu hii, sijawahi kuona kisa kama hicho ambacho
kilipangwa na kutekelezwa kwa umaakini huo.''
Mkewe mwanamume huyo mwenye watoto watatu , pia alikuwemo
kwenye sakata kwani siku zote alionekane akimhudumia mumewe aliyejidai kuwa
hali mahututi. T
Mbunge wa eneo la Swansea West aliambia BBC kuwa: "Nilikutana
na Bi Hellen na akaniarufu ambavyo mumewe alikuwa na hali mbaya ya kiafya na
kwamba walitendewa vibaya na polisi.''
Knight anakabiliwa na mashitaka 19 ikwemo wizi na ikiwa
atapatikana na hatia huenda akafungwa jela.
No comments:
Post a Comment