Mwanajeshi wa kikosi maalum cha wanamaji kuitoka jeshi la China, akionyesha matumizi ya mikono dhidi ya adui, wakati wa uzinduzi wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Wanamaji wa China na Tanzania kwenye kamandi kuu ya kikosi cha wanamaji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Jumanne Oktoba 21, 2014. Mazoezi hayo yaliyopewa jina "Surpassing 2014" yalianza kwa maonyesho ya matumizi ya mikono katika kupambana na adui pamoja na maonyesho ya zana za kivita ambapo Mkuu wa Operesheni na mafunzo wa JWTZ, Meja Jenerali James Mwakibolwa, na Meja Jenerali Wu Xiao Yi kutoka vikosi vya wanamaji vya China, ndio waliozindua mazoezi hayo baada ya kusaini makubaliano ya kufanya hivyo |
No comments:
Post a Comment