Pia inaarifiwa huwa na busara zaidi kufidia kimo chao,
amekiri Adam Gopnik, mwanamme mmoja wenye umbo dogo.
Wiki kadhaa zilizopita, wana soshologia wawili kutoka Chuo
Kikuu cha New York, walichapisha waraka mrefu ulioangalizia maisha ya watu
wafupi.
Utafiti wao ulizua mjadala mkali kutoka kwa kile kinachoweza
kusemekana kuwa jamii ya wanaume wenye kimo kifupi.
Waandishi wa waraka huo wa maswala ya kijamii unaashiria
kwamba wanaume wenye haiba ya kuvutia mara nyingi hupendelewa katika maisha yao
hivyo wanaripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja.
Hata hivyo, hitimisho la waraka huo, pindi mtu
anapoupitia, unashangaza. Ni kwamba, watu wafupi wana ndoa za kudumu zaidi
Wanafanya hayo, katika mazingira magumu wakiwa katika umri
tofauti na kipato tofauti, na wanayafanya hayo wakiwa na wanawake wafupi ambao
wanawaoa, na wakati mwengine na hata wanawake warefu wanaokutana nao.
Wanaume wafupi wanaoa kuchelewa, lakini pindi wanapooa,
wanadumu katika ndoa kwa muda mrefu, na kwa kiwango cha sayansi ya kijamii, angalau
wanakuwa na furaha.
Kuna sababu zinazoonyesha kwa nini wanaume wafupi wanadumu
kwenye ndoa.
Nazo ni, wanaume wafupi wanaonyesha kukata tamaa. Wanaume
wafupi wanaishi katika ulimwengu wa wanaume warefu na wanajua kila fursa
inayopatikana, ni bora kuidhibiti.
Hali ya kukata tamaa ndio inayowafanya wanaume wafupi kuwa
wanaume bora kwa wake zao. Watafiti hao pia walisema kuwa wanaume wafupi
hukimbilia kufanya kila kitu kuwafurahisha wapendwa wao wakati wanume warefu
hilo halliwajalishi.
Moja wapo ya ufumbuzi wa ripoti hiyo pia ni kwamba wanaume
wafupi wanafanya kazi chache za nyumbani wanapokuwa kwenye ndoa kuliko wanaume
warefu, ingawa utafiti pia unaonyesha kwa wanaume wenye kimo kirefu, aina ya
kazi zao za nyumbani inatofautiana.
Kwa maana nyengine, wanaume wafupi hawafiki juu ya makabati.
Wanaume wafupi hawadumu kwenye ndoa kwa sababu ya kutaka kuridhisha, bali
wanadumu kwenye ndoa kwa sababu wanataka kuonekana.
Utafitio huu kama ulivyosoma hapo awali umeua mjadala mkali
lakini pindi mtu anaposoma utafiti wao kinachojitokeza zaidi ni kuwa wanaume
wafupi wanakuwa na ndoa za kudumu.
Hii ni licha ya mazingira magumu wanayokabiliwa nayo katika
ndoa zao na hufanya hivyo na wake wafupi waliowaoa lakini pia na wanawake
warefu wanaokuwa wamewaoa.
Utafiti huo unahitimika kwa kusema wanaume wafupi hawana
kasi ya kuoa lakini wanapooa wao hudumu katika ndoa zao.
No comments:
Post a Comment