Mama akimuaga marehemu mwanaye, Method Clecence Mengi.
MAMIA ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakiongozwa na
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude
wamejitokeza kumzika marehemu Method Clecence Mengi aliyeuawa kwa kuchomwa visu
na watu wasiofahamika nchini Marekani.
Mengi alikumbwa na ukatili huo wa kuchomwa visu vitatu,
tumboni viwili na kwenye paji la uso Septemba 17, mwaka huu nje ya nyumba yake,
Texas nchini humo na watu hao bila kujulikana kisa na waliingia mitini baada ya
tukio hilo la kikatili.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu
Telesphor Mkude akiuombea mwili wa marehemu Method Clecence Mengi. Mara baada
ya tukio hilo, mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi
kwenda hospitali kwa
uchunguzi mpaka Oktoba 1, mwaka huu ulipotolewa na kuletwa nchini kwa mazishi.
Mwili wa Mengi aliyeishi nchini Marekani tangu mwaka 2000,
uliwasili nyumbani kwa wazazi wake, alfajiri ya Oktoba 2, mwaka huu na baadaye
saa tisa alasiri kupelekwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Patrick kwa ibada ya
mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Waombolezaji wakiupokea mwili wa marehemu Method Clecence
Mengi kwa ajili ya mazishi Marehemu alizikwa saa kumi kwenye Makaburi ya Kolla
huku akiacha maswali ya namna alivyouawa na mkewe ambaye ni Mmarekani
kutoonekana kwenye mazishi wala kuja Bongo.
Akizungumza baada ya mazishi hayo, mdogo wa marehemu Ribbon
Mkali ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilakala alisema:
Marehemu Method Clecence Mengi (kushoto) enzi za uhai wake
”Ni kweli shemeji yangu, mke wa marehemu hajafika nchini bado yuko Marekani na
watoto wake wawili, zaidi ngoja tumalize msiba, tutaongea mengi.”
No comments:
Post a Comment