Idara ya haki imekiri kwamba mmoja wa maajenti wake alibuni
ukurasa huo wa mtandao wa facebook bila kumuelezea Sondra Arquiett.
Hapo awali idara hiyo ilisema kuwa bi Arquiett alikubali
hatua hiyo kwa kuwa aliwaruhusu maafisa wake kuingia katika simu yake ya
mkononi.
Idara hiyo ya haki sasa inachunguza iwapo ukurasa huo ni
ukiukaji wa haki za mwanamke huyo.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa wiki ijayo mjini New York
,huku serikali ya Marekani na ajenti huyo wa kitengo cha kukabiliana na dawa za
kulevya Timothy Sinnigen wakitajwa kuwa washtakiwa.
Mtandao huo bandia ulibuniwa baada ya muhudumu huyo wa
mgahawa bi Arquiett kukamatwa mnamo mwezi Julai 2010,na kushtumiwa kwa kuhusika
katika genge moja la dawa za kulevya.
Alikiri njama ya kumiliki dawa ya Cocaine kwa lengo la
kuisambaza na alihukumiwa miezi sita ya kifungo cha wikendi.
Wakati alipokamatwa ,bi Arquiett alisalimu simu yake ya
mkononi na kuwaruhusu maafisa kuchunguza data yake ili kuwasaidia na uchunguzi
wa uhalifu kama huo.
Uchunguzi huo ulimshirikisha mpenziwe,Jermaine Branford
ambaye alishukiwa kwa kuratibu uuzaji wa dawa za kulevya.Baadaye alikiri kuwa
katika njama ya kuuza dawa hizo za kulevya.
Bi Arquiett hatahivyo alisema kuwa hakuelezwa iwapo
oparesheni hiyo ingebuni ukurasa bandia wa facebook kupitia jina la Sondra
Prince ambalo amekuwa akiitwa na marafikize.
Ukurasa huo ulishirikisha picha za mwanamke huyo pamoja na
zile za mwanawe na mpwa wake.
Kulingana na wakili wake picha moja ilimuonyesha mwanamke
huyo akiwa nusu uchi.
Bi Arquiett amesema kuwa hatua hiyo inakiuka haki zake za
faragha na sasa anataka kulipwa fidia ya dola 250,000.
No comments:
Post a Comment