Atto Mensah amesisitiza kuwa yeye ndiye mkufunzi wa timu ya
soka ya Sierra Leone licha ya ripoti kwamba John Sesay Ajina ameteuliwa kuwa
kocha mpya wa kikosi hicho.
Sesay aliajiriwa ili kusimamia kikosi hicho dhidi ya
Cameroon katika mechi ya kufuzu kwa kombe la taifa bora barani afrika.
Shrikisho la soka nchini Sierra Leone linaamini kuwa
Mensah
hajafuzu kusimamia michuano hiyo ya tarehe 11 na 15 mwezi Octoba.
lakini Mensah ameiambia BBC kwamba anaamini amefuzu
kusimamia kikosi hicho na kwamba ametoa stakhabadhi zake zote kwa shirikisho
hilo kuonyesha masomo ya ukufunzi aliyofanya. . Anasema kuwa amefanya mazoezi
na kikosi hicho na yuko tayari kukiongoza.
Mensah aliteuliwa na shirikisho la soka nchini Sierra Leone
pamoja na wizara ya michezo mnamo mwezi Septemba baada ya Johnny Mc Kinstry
kufutwa kazi.
Lakini Shirikisho hilo linasema kuwa limemfuta kazi na
nafasi yake kuchukuliwa na Sesay kama kaimu kocha ,huku Abdulai Bah akiwa naibu
wake na kwamba wawili hao wanatarajiwa kuwasili mjini Younde siku ya alhamisi
ili kuanza kuiongoza timu hiyo.chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment