TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti
la Raia Mwema la wiki hii ya Oktoba 8-14 ambalo limetolewa juzi,
Jumatano, Oktoba 8, 2014, limeandika kwenye ukurasa wake wa kwanza
habari yenye kichwa cha habari, “Mwekezaji aliyemzawadia saa Kikwete
aibua utata”.
Kichwa
cha habari hicho kinafuatiwa na habari yenyewe ambayo kwenye moja ya
aya zake inadai kuwa “tayari Rais Kikwete amekutana na mwekezaji huyo wa
Marekani, Bwana Roberk Shumake na kumpa zawadi ya saa aina ya Rolex
katika mojawapo ya ziara za Rais nchini Marekani”.
Hii ni habari ya uongo na haiwezi kuwa ya uongo zaidi kuliko
ilivyochapishwa.
Hii ni habari ya uongo na haiwezi kuwa ya uongo zaidi kuliko
ilivyochapishwa.
Ni
habari ya uzushi na upuuzi. Ni habari inayolenga kumdhalilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwamba
amepokea zawadi kutoka kwa mtu ambaye anajaribu kupewa kandarasi
kujenga usafiri wa treni jijini DSM na ambaye pia anahusishwa kwenye
shughuli nyingine za kibiashara zenye utata huko kwao Marekani.
Rais Kikwete hakuwahi kupewa wala kupokea saa ya aina ya Rolex kutoka kwa Bwana Shumake ama kutoka kwa mfanyabiashara mwingine yoyote.
Rais Kikwete hakuwahi kupewa wala kupokea saa ya aina ya Rolex kutoka kwa Bwana Shumake ama kutoka kwa mfanyabiashara mwingine yoyote.
Alichopewa
Mhe. Rais na Balozi huyo wa Heshima anayewakilisha Tanzania katika
jimbo la Michigan ni saa ya kumbukumbu ya mji wa Detroit ambako ndiko
nyumbani kwa Bw. Shumake (Souvenir watch), sio saa ya aina ya Rolex kwa
matumizi binafsi ya Mhe. Rais. Saa hiyo ya kumbukumbu ni mali ya
Tanzania.
Na wala siyo
hulka wala tabia yake ya kupokea zawadi kutoka kwa watu wanaotafuta
fursa za kuwekeza katika Tanzania. Isitoshe kwa nafasi yake kama Rais
hahitaji kupewa saa na watu wa nje kwa sababu mahitaji yake yote ya
mavazi na mengine hutolewa kwake na Taifa analoliongoza.
Ni
jambo la kusikitisha sana kuwa gazeti la hapa nyumbani linaweza, bila
ushahidi wowote na kwa kukariri habari kutoka kwenye mitandao ya
kijamii, kuamua kuchapisha habari yenye kulenga kumdhalilisha kiongozi
wa Taifa letu, tena kwa kumhusisha na zawadi ya kipuuzi kama saa aina ya
Rolex.
Ni matarajio yetu
kuwa Gazeti hilo litaombwa kutoa ushahidi wa habari hiyo, ili kuondoa
utata ambao dhahiri utajitokeza kutokana na kuchapishwa kwa habari hiyo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Oktoba, 2014.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Oktoba, 2014.
No comments:
Post a Comment