Komandoo Octavian Mgowele mwenye cheo cha Luteni wa Kikosi
cha 94 KJ Ngerengere,
Morogoro, Oktoba 13, mwaka huu alidaiwa kumuua Aron kwa
kumpiga kipigo kibaya.Tukio hilo lilidaiwa kutokea kwenye baa iitwayo Mbondela
iliyopo Yombo - Buza maeneo ya Kipera, jijini Dar kwa madai kwamba alikuwa
akimbughudhi mke wa komandoo huyo. Taarifa toka kwa mtu aliyekwepo kwenye baa
hiyo zinasema siku hiyo mjeshi huyo alikaa meza moja na mkewe ambaye alitoka
kufunga naye ndoa jana yake. Pia kwenye meza hiyo alikaa Aron huku wakiendelea
kunywa bia ambapo mnunuaji mkuu alikuwa komandoo.
Marehemu Aron Kihundwa enzi za uhai wake.Ikadaiwa kuwa, kuna
wakati komandoo alikwenda kaunta aliporudi alishangaa kumkuta mkewe amehama
katika kiti alichomuacha. Chanzo hicho kikaendelea kusema komandoo huyo
alimuuliza mkewe kisa cha kuhama kiti, naye akamjibu; si huyu rafiki yako
ananisumbua.’
Wakati huo, marehemu alikuwa anauchapa usingizi kutokana na
kulewa.
“Marehemu akiwa usingizini alishtukia komandoo akimwadhibu
bila kujua sababu ni nini hadi akamjeruhi.
”Baada ya kumpiga sana hadi kumjeruhi tulimchukua marehemu
na kumpeleka Kituo cha Polisi Chang’ombe (Dar) na kupewa PF3, tukamkimbiza
Hospitali ya Temeke, ilipofika saa kumi usiku wa kuamkia kesho yake alifariki
dunia.
“Aron ni rafiki yake sana komandoo, hata siku ya ndoa yake,
yeye ndiye aliyempambia gari la harusi na ukumbi. Siku ya tukio ilikuwa ni
sherehe ya kuvunja kamati.
“Hatujajua ni kwa nini komandoo aliamua kumpiga Aron kiasi
kile, mambo ya kuambiwa na mwanamke siyo ya kuyafanyia kazi kama haukushuhudia
ama hauna uthibitisho,” alisema shuhuda huyo.
Marehemu Aron alizikwa Oktoba 18, mwaka huu kijijini kwao
Kyengia Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.HABARI NA GPL (GLOBAL PUBLISHERS)
No comments:
Post a Comment