Mahakama ya kimataifa ya ICC, imeonya serikali ya Kenya
dhidi ya kufichua taarifa kuhusu kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta kwa
vyombo vya habari nchini humo.
Rais Kenyatta amekuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika
katika mahakama ya ICC kusikiliza kesi inayomkabili mapema mwezi huu.
Anakana madai anayokabiliwa nayo ya ukiukwaji wa haki za
binadamu pamoja na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Lakini mahakama inasema kuwa ina wasiwasi kuhusu
serikali
Kenya kuweza kuficha taarifa kuhusu Kesi ya Kenyatta.
Katika ripoti yake iliyotolewa Jumanne, mahakama hiyo
iligusia hatua ya kufichuliwa kwa maelezo au ombi la siri lilitolewa na majaji
kwa serikali ya Kenya kuisaidia kupiga tanji mali ya Rais Kenyatta.
Ombi hilo lilitolewa kwa njia ya kisiri hata hivyo maafisa
wakuu wa Kenya waliwasilisha stakabadhi hadharani kuhusu ombi hilo lililotolewa
mwaka 2013 ingawa mawakili wa Kenyatta waliomba radhi kwa hilo.
Upande wa mashitaka unasema serikali ya Kenya imebana
ushahidi unaohitajika na mahakama hiyo
Maelezo ya ombi hilo tena yalijitokeza katika vyombo vya
habari nchini Kenya kati ya mwezi Aprili na Septemba, mwaka huu katika kile
ambacho mahakama imesema ni uvujaji wa taarifa za siri kwa vyombo vya habari
hata kabla ya mahakama kujulishwa.
Mahakama hiyo imetoa onyo kwa Kenya kwa kutotii mahakama.
Kenyatta anakabiliwa na makosa 5 kuhusiana na ghasia za
baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 ambapo watu 1,200 waliuawa na wengine
laki sita kuachwa bila makao katika ghasia mbaya zaidi kuwahi kushuhuhdiwa
nchini Kenya tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka 1963.
Tarehe 8 mwezi Oktoba alitakiwa na mahakama kufika ICC kwa
kikao maalum.
Lakini wadadisi wanasema kuwa kesi hiyo imegonga mwamba
upande wa mashitaka ukituhumu serikali ya Kenya kwa kubana ushahidi
unaohitajika na mahakama hiyo huku utetezi ukisema bila ya ushahidi kesi hiyo
haipaswi kuendelea.
No comments:
Post a Comment