Kulala na wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na
ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo,kulingana na utafiti.
Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la
saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal wamebaini kwamba
ikilinganishwa na wanaume walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala
na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa kupatikana na ugonjwa huo kwa
asilimia 28.
Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo
kati yao
Wanaume 1,590 walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti
mwaka 2009.
Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye
saratani ya kibofu cha mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa
familia zao wenye saratani.
Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi
wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha
yake,tisho la kupata ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia
19 kwa aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne
wa kiafrika hupatikana na saratani
No comments:
Post a Comment