Mama mmoja mkazi Mabwepande wilaya ya
Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam amevamia kituo cha ITV
akiwa na watoto mapacha sita kulalamikia kuishi maisha ya tabu na watoto
wadogo baada ya kutelekezwa na mumuwe kwa madai ya kuzaa kupita kiasi.
Akizungumzia maisha yake mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Salome Paulo Mhando mkazi wa Mabwepande, amesema mume wake amemtelekeza
na kumuacha na watoto mapacha sita kwa madai ya kuzaa watoto mapacha
kila anaposhika ujauzito na kusababisha familia kuwa kubwa kupita kiasi
huku akijua wazi kuwa kupata mapacha ni mipango ya mungu.
Kutokana na kuishi katika maisha ya mateso ameomba wasamaria wema
kujitokeza kumsaidia ili aweze kupata mavazi, chakula na matibabu ya
watoto huku akisisitiza kusaidiwa kupata mtaji wa kufanya biashara ya
mkaa hivyo yeyote atakayeguswa afikishe msaada wake katika kituo cha ITV
Mikocheni jijini Dar es salaam au atume mchango wake kupitia Tigo pesa
0715 358535.
No comments:
Post a Comment