Pages

Friday, October 31, 2014

MAMA HUYU AKIMBIWA NA MUMEWE HUKO MABWEPANDE KUTOKANA NA KUZAA OVYO WATOTO WENGI


Mama mmoja mkazi Mabwepande wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam amevamia kituo cha ITV akiwa na watoto mapacha sita kulalamikia kuishi maisha ya tabu na watoto wadogo baada ya kutelekezwa na mumuwe kwa madai ya kuzaa kupita kiasi.

Akizungumzia maisha yake mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Salome Paulo Mhando mkazi wa Mabwepande, amesema mume wake amemtelekeza na kumuacha na watoto mapacha sita kwa madai ya kuzaa watoto mapacha kila anaposhika ujauzito na kusababisha familia kuwa kubwa kupita kiasi huku akijua wazi kuwa kupata mapacha ni mipango ya mungu.



Kutokana na kuishi katika maisha ya mateso ameomba wasamaria wema kujitokeza kumsaidia ili aweze kupata mavazi, chakula na matibabu ya watoto huku akisisitiza kusaidiwa kupata mtaji wa kufanya biashara ya mkaa hivyo yeyote atakayeguswa afikishe msaada wake katika kituo cha ITV Mikocheni jijini Dar es salaam au atume mchango wake kupitia Tigo pesa 0715 358535.

No comments:

Post a Comment