Pages

Saturday, October 25, 2014

MWANDOSYA AMUWAKILISHA JK SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA ZAMBIA

unnamedWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya  akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo.
unnamed3Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya (wa tatu kulia ) pamoja na Mkewe Lucy Mwandosya wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa wa Zambia wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Wengine kutoka kulia ni Kaimu Rais wa Zambia Mhe Edgar Lungu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, na wa  pili kulia ni Makamu wa Rais wa Nigeria Monance Namadi Sambo. 

 unnamed5Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya  na mkewe Lucy Mwandosya wakisalimiana na Rais wa kwanza wa Zambia Mzee Kenneth  Kaunda wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo ambazo zimefanyika Mjini Lusaka jana.
Picha na Mpiga Picha wetu

No comments:

Post a Comment