Rais Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014.
Vifijo baada ya ufunguzi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa mfanyakazi wa Hoteli
ya Diaoyutai iliyoko Beijing mara baada ya kuwasili hotelini hapo. Mama
Salma ameambatana na mumewe Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye amewasili
nchini China tarehe 21.10.2014 kwa ziara ya kiserikali.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya
mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi
tarehe 21.10.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang Hua, Mmoja wa
viongozi wakuu wa China National Offshore Oil Corporation (CNOOC),
wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa
Shirika hilo Bwana Wang Yilin kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea
makao makuu ya Shirika hilo yaliyoko Beijing nchini China tarehe
22.10.2014. Shirika hilo hujishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi
baharini, uchimbaji na uuzaji wa maliasili hizo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika kumbukumbu yake kwenye kijiji cha sanaa za Afrika mara baada ya Rais Dkt. Kikwete kuandika kumbukumbu yake.
Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong wakimkabidhi zawadi ya mchoro wa Tingatinga Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe 22.10.2014. Picha na John Lukuwi.
No comments:
Post a Comment