Polisi mjini Nairobi wamewakamata watu 100 katika msako
baada ya mwanamke mwingine kuvuliwa nguo katika mtaa wa mabanda wa Kayole mjini
Nairobi.
Inadaiwa mwanamke huyo alikuwa amevalia nguo zisizo za
heshima.
Naibu kamanda wa polisi mjini Nairobi Moses Ombati,
amaenukuliwa akisema wengi wa waliokamatwa walikuwa wanaume walevi.
Bwana Ombati aliongeza kusema kwamba, mwanamke huyo
alishambuliwa katika mtaa wa Kayole Jumatatu jioni na kwamba polisi wanaendelea
na msako.
Mnamo Jumatatu mamia ya wanawake waliandamana katika
barabara za katikati mwa mji kulaani kitendo cha kumvua nguo mwanamke mwingine
mapema mwezi huu mjini Nairobi.
Wanawake hao waliandamana kufuatia wito kwenye mitandao ya
kijamii chini ya kauli mbiu #MyDressMyChoice yaani vazi langu uamuzi wangu au
nitavaa nitakachojiamulia mwenyewe.
Waandamanaji hao wakiwemo wanawake mashuhuri, wanasiasa na
wanaharakati waliandamana hadi katika kituo cha mabasi ambako mwanamke wa
kwanza alidaiwa kuvuliwa mavazi yake kwa madai alikuwa amevalia 'Mini Skirt'
No comments:
Post a Comment