Kijana mmoja Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu
Dar, juzi kati alijilipua na mafuta ya
taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa na babu yake. Tukio hilo lilitokea eneo la
Makongo Juu Makaburini usiku ambapo kijana huyo na babu yake aliyemtaja kwa
jina moja la Mhagama waligombana.
Kijana Nicholas Mhagama (25) aliyejilipuwa na mafuta ya taa
akidai kunyanyaswa.
|
Baada ya kijana huyo kuona isiwe tabu alijilipua na mafuta
ya taa alipoona maumivu yanazidi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada ambapo
aliokolewa na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala na baadaye kuhamishiwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuwa mbaya.
Waandishi walikwenda kufanya mahojiano naye hospitalini hapo
ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ndugu zangu naomba
mnisaidie nipone kwani uamuzi niliouchukua haukuwa sahihi ni hasira za kilevi
nilichokuwa nimekunywa.
“Yote haya ni sababu ya manyanyaso niliyopata kutoka kwa
babu yangu ambaye alinifukuza nyumbani na kunitaka nikapange nyumba wakati
nilikuwa na matatizo ambayo alikuwa akiyajua,” alisema Mhagama.
Aliongeza: “Niliwahi kukutwa na ajali mbaya ambayo ilisababisha
niende kuishi nyumbani kwa bibi yangu ambapo babu amekuwa kero. “Awali
nilipofika nyumbani sikumkuta babu lakini alipofika akawa kero kwangu kwani ni
mtu anayetaka nimpe hela kila kukicha, nilikuwa nikienda kuhangaika napata elfu
ishirini nampa elfu kumi na tano na mimi naweka elfu tano kwa ajili ya
kujipanga ili nikapange chumba.
ALIAMBIWA AKICHELEWA ATAFUNGIWA MLANGO
“Siku ya tukio nilimuaga naenda kwa baba yangu mdogo
kumsalimia akaniambia nikirudi usiku nitakuta amefunga mlango nitafute pa kwenda
kulala.
“Kweli, niliporudi alianza kuninyanyasa kwa maneno, ugomvi
wetu ukawa mkubwa nikaona bora nijiondoe duniani kwani siwezi kuendelea kuishi
maisha ya manyanyaso kama haya,” alisema Nicholas kwa shida kutokana na
majeraha aliyonayo mwilini hasa usoni na mikononi.Nicholas Mhagama akiuguza
majeraha hospitalini.
Akizungumza kwa njia ya simu bibi wa kijana huyo, Bi.
Mhagama alikiri kwamba ni kweli huyo babu ambaye yeye anamuita shemeji amekuwa
akimnyanyasa sana Nicholas. “Ni kweli amekuwa akimfukuza nyumbani hapo wakati
siyo kwake na siku ya tukio baada ya kuona ugomvi umekuwa mkubwa nilikimbilia
kwa mwanangu huko Kimara.
“Ugomvi kati ya babu yake huyo mdogo na huyu Nicholas ulianza saa tatu usiku.
Nilipoona kero niliamua kutimkia Kimara kwa mwanangu,” alisema bibi huyo.
SIMU YA MOTO YAPIGWA USIKU
“Ilipotimia saa nne usiku nikapigiwa simu na kufahamishwa
kuwa Nicholas kajilipua kwa mafuta ya taa.
BABU ORIJINO ALISHAFARIKI
“Mume wangu (Babu orijino) alishafariki na huyu Nicholas
kweli kabisa huwa anagombana na huyo
babu ambaye ni shemeji yangu. “Kisa cha ugomvi wao ni kumpa manyanyaso ya hali
ya juu, nawaomba mumsaidie huyo kijana, naombeni jamani,” alisema bibi huyo.
Juhudi za kumpata babu huyo anayedaiwa kumnyanyasa mjukuu
wake hazikuzaa matunda.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment