Gari ya chuo kikuu cha Iringa zamani Tumaini limepata ajali
mbaya na kusababisha vifo vya watu wawili. Gari hii ilikuwa imetoka kumpokea
Lecturer mgeni (volunteer toka Ujerumani).Wakiwa wanarudi kuelekea chuoni kuna
muendesha baiskeli alikatiza barabara ghafla na katika jitihada za kumkwepa
gari ilipoteza muelekeo na kupinduka.
Hata hivyo muendesha baiskeli huyo aligongwa na kufa papo
hapo na wengine kujeruhiwa.Wakati wakipelekwa hospitalini Lecturer toka
ujerumani aliyekuja kujitolea kufundisha naye alifariki hivyo kufanya idadi ya
vifo kufikia 2.
Ajali hii imetokea kama saa 11 jioni ya jana eneo la mtandika
kama km 10 hivi Mbele ya Hotel ya AL Jazeera ukitokea Dar.
No comments:
Post a Comment