Pages

Friday, November 7, 2014

Ajali mbaya: Gari ya chuo kikuu Tumaini Iringa na kuua wawili

Gari ya chuo kikuu cha Iringa zamani Tumaini limepata ajali mbaya na kusababisha vifo vya watu wawili. Gari hii ilikuwa imetoka kumpokea Lecturer mgeni (volunteer toka Ujerumani).Wakiwa wanarudi kuelekea chuoni kuna muendesha baiskeli alikatiza barabara ghafla na katika jitihada za kumkwepa gari ilipoteza muelekeo na kupinduka.

Hata hivyo muendesha baiskeli huyo aligongwa na kufa papo hapo na wengine kujeruhiwa.Wakati wakipelekwa hospitalini Lecturer toka ujerumani aliyekuja kujitolea kufundisha naye alifariki hivyo kufanya idadi ya vifo kufikia 2.


Ajali hii imetokea kama saa 11 jioni ya jana eneo la mtandika kama km 10 hivi Mbele ya Hotel ya AL Jazeera ukitokea Dar.

No comments:

Post a Comment