Pages

Monday, November 17, 2014

ASKOFU CHARLES GADI, AONGOZA IBADA YA KUMUOMBEA RAIS JAKAYA KIKWETE NAFUU YA HARAKA

Askofu wa kanisa la Good News for All Ministry, Charles Gadi, (Wapili kulia), na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ahmed Kipozi, wakiwa kwenye maombi ya kumuombea rais Jakaya Kikwete, apone haraka na kurejea nyumbani kuendelea na majukumu yake ya kitaifa. Rais yuko nchini Marekani kwa matibabu ya tezi dume, na tayari ameruhusiwa kutoka hospitali aliyokuwa akitibiwa
Askofu wa kanisa la Good News for All Ministry, Charles Gadi,(Wanne kushoto0, akiaongoza wananchi akiwemo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo 



mkoani Pwani, Ahmed Kipozi, (Kushoto kwake), kwenye ibada maalum ya kumuombea rais Jakaya Kikwete, apone haraka. Ibada hiyo ilifanyika kwenye kijiji cha Mapinga wilayani humo leo Jumapili Novemba 16, 2014. Rais Jakaya Kikwete yuko nchini Marekani kwa matibabu ya tezi dume, na tayari alikwisha fanyiwa operesheni na kuruhusiwa kutoka hospitalini baada ya hali yake kuimarika. Kwa mujibu wa Ikulu, kwa sasa rais bado yuko huko akipatiwa uangalizi wa kimatibabu nje ya hospitali.

Picha kwa hisani ya K-VIS Production

No comments:

Post a Comment