Pages

Monday, November 17, 2014

Burkina Faso yapata rais wa mpito

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Burkina Faso Michel Kafando, ametajwa kuwa rais wa mpito nchini humo.
Jitihada zimekuwa zikiendelea nchini humo kumchagua kiongozi wa mpito kufuatia kuidhinishwa hapo jana na jeshi na viongozi wa mashirika ya kiraia kwa mpango wa mwaka mzima utakaohakikisha kufanyika uchaguzi.
Kafando alikuwa mmoja kati ya watu wanne ambao wangechukua wadhifa huo, wakiwemo waandishi 


wawili na msomi mmoja.
Viongozi wa mashirika ya kiraia na wawakilishi wa jeshi walishughulika hadi usiku katika mji wa Ouagadougou kuamua nani atachukua wadhifa huo wa rais wa mpito.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya mpito, ilikuwa ni lazima awe raia ambaye hatogombea katika uchaguzi huo.

Mwishowe walimchagua raia aliyependwa zaidi na jeshi, mwenye umri wa miaka 72 na waziri wa mambo ya nje wa zamani Michel Kafando, Sasa ni lazima amchague waziri mkuu ambaye anaweza kuwa raia au afisa wa jeshi kuongoza serikali ya watu 25 ya mpito.

No comments:

Post a Comment