Stori: Chande Abdallah, Deogratius Mongela na Musa Mateja.
TENA! Saa chache tu baada ya Miss Tanzania 2014 aliyezua
tafrani la kuchakachua umri kwa kujipunguzia miaka 2 ya kuzaliwa, Sitti Abbas
Mtemvu kujisalimisha kwa kujivua taji mwenyewe, mapya yameibuka na Ijumaa
Wikienda lina mzigo mkononi!
Mapya hayo yameibukia ndani ya Kanisa la Revelation Church
lililopo Buza–Kipera jijini Dar kwa Nabii Yaspi Bendera ambaye amezungumzia
ishu ya Sitti kujivua taji
mwenyewe.“Alikuja kwangu nikamwombea, akapata taji. Hata alipopata alikuja
kushukuru, nilimwambia aendelee kudumu kwangu hadi atakapokwenda kwenye taji la
dunia (Miss World) lakini hakufanya hivyo, akawa haji tena.“Hivi, nitoe mfano
mmoja. Kama mtu akienda kwa mganga kuomba apewe dawa ili apate ujauzito, akishapata
akaenda kwa mganga mwingine kuomba amfanyie dawa ili ujauzito huo usitoke. Je,
siku ukitoka nani analaumiwa, mganga wa kwanza au wa pili?”
Aliyekuwa
Miss Tanzania 2014 akipokea maombi ya nguvu kutoka kwa Nabii Yaspi Bendera
No comments:
Post a Comment