Ndege hiyo ikisukumwa
Abiria waliokuwa wanafanya safari na shirika ka ndege la
Serbia walilazimika kushuka katika ndege hiyo na kuisukuma baada ya breki zake
kuganda na kushindwa kuondoka.
Ndege hiyo ilikuwa inaanza kuruka kutoka katika mji wa
Kirusi wa Igarka,lakini ilishindwa kusogea baada ya hali ya hewa kuwa -52C.
Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo idadi yao kubwa
walikuwa wafanyakazi wa ndege hiyo
waliombwa kutoa msaada wa dharura wa
kuisukuma ndege hiyo kwa hofu ya kutowachelewesha endapo watasubiri msaada
Zaidi.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Katekavia baada ya muda
ilimudu kuendelea na safari zake na baadaye kutua salama katika mji wa
Krasnoyarsk.kwa muujibu wa mashuhuda wa tukio hili kiwango cha baridikwa
muujibu wa mashuhuda wa tukio hili ,wanaeleza kuwa kiwango cha baridi kilishuka
hadi kufikia nyuzi joto 52, na kugandisha mfumo wa breki za ndege hiyo .
Mkuu wa kitengo cha huduma za ndege hiyo Oxana Gorbunova,
anaeleza kwama abiria hawakulazimishwa kuisukuma ndege hiyo bali kwa hiyari
waliamua kusaidia kuisukuma ,japokuwa kitendo hicho hakiruhusiwi kwakuwa
kitendo hicho kinaweza kuathiri bodi ya nje ya ndege hiyo ,na wanasheria nao
wanachunguza endapo uwanja wa ndege,shirika la ndege,wafanyakazi wa ndege ama
abiria endapo wamevunja sheria za usalama wa anga.
Uwanja huo wa ndege unatumiwa na abiria takribani elfu moja
kwa mwaka ,wengi wao hufanya kazi katika makampuni ya mafuta yanayomilikiwa na
Urusi.
No comments:
Post a Comment