Basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria40 ‘Bio bus’ linatumia
gesi itokanayo na kinyesi cha binadamu na takataka nyingine zinazozalishwa
kwenye kiwanda kilichopo kusini Magharibi mwa nchi hiyo kuweza kutembea.
Katika Gazeti la UHURU limeandika kuwa tanki moja la gesi
hiyo lililozalishwa kutokana na kinyesi cha watu inatosha kuendesha gari hilo
kwa umbali wa kilomita305.
Basi hilo rafiki wa mazingira ambalo watengenezaji wake
wanasema litaboresha hewa, linaendeshwa kwa nishati ambayo ni ya
kawaida,kinyesi cha binadamu ambacho ni miongoni mwa majitaka mengine.
Watengenezaji hao walisema gari hilo la aina yake
litaboresha hali ya hewa na kuthibitisha kumbe kuna thamani katika kinye si cha
binadamu.
Zipo taarifa kuwa siku si nyingi kinyesi cha binadamu
kitaanza pia kuzalisha nishati kwa ajili ya simu za mkononi baada ya wataalam
kutoka chuo kikuu cha East Anglia cha nchini humo.
Gesi hiyo inazalishwa katika mtambo wa majitaka wa Wessex
Water,unaendeshwa na kampuni ya nishati ya Geneco na ugunduzi ,huo unaweza
kuzalisha
nishati kwa ajili ya teknolojia inayobebeka kama vile simu za mkononi
na hata kompyuta mpakato.
Watetezi wa nishati hiyo wanasema basi hilo ambalo
linatarajia kusafirisha abiria 10,000 kwa mwezi,linaonyesha thamani ya takataka
na linaonyesha mustakabali mwema katika sekta ya usafiri wa umma.
No comments:
Post a Comment