Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 19, 2014

EPUKANA NA STRESS, HAYA NDIO MADHARA KUMI(10) YATOKANAYO NA STRESS




  1. “Stress” hukufanya uzeeke mapema
  2. Hupunguza uwezo wa kufikiri. “Stress” hufanya ubongo kuwa dhaifu katika kufikiri.
  3. Hupelekea kupoteza kumbukumbu na pia uwezo wa kutunza vitu vipya kichwani hupungua.
  4. “Stress” hupambana na mfumo wa ulinzi wa mwili na hivyo kukufanya uwe katika hatari kubwa ya kupata magonjwa tofauti na mtu asie na “stress” sana.
  5. “Stress” huzipa uhai seli zinazosababisha kansa mwilini na hivyo kukufanya kuwa na hatari zaidi ya kupata kansa.
  6. Huharibu “mood” yako na kukufanya muda wote kuwa ni mtu wa huzuni tu.
  7. Husababisha ngozi ya mwili kuzoofika. “Stress” huzalisha homoni iitwayo “glucocorticoid” ambayo huzoofisha ngozi na pindi “stress” zikiisha na yenyewe hukata.
  8. Huathiri afya ya meno kwa sababu watu wengi huishia kusugua meno yao pindi wakiwa na “stress”.
  9. Husababisha maumivu makali ya kichwa na hii ni kutokana na mawazo sana na kichwa huwa kimebeba mzigo mzito mno.
  10. Hupunguza mvuto wa kufanya mapenzi na ni mbaya sana hasa kwa wale walio katika ndoa kwani hupelekea kutokufurahia tendo la ndoa kabisa na pia huweza pelekea kuvunjika kwa ndoa.

No comments:

Post a Comment