Pages

Thursday, November 27, 2014

JIONEEE: WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. MUHONGO ATOA UTETEZI WA SERIKALI BUNGENI

 Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
 Ameanza kwa kuomba radhi kama jana kulikuwa na usumbufu wa umeme na anawaagiza mameneja wote wa TANESCO wasikate umeme.
 Anatoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow, mengi yamesemwa na ni wakati wa kuanza mjadala kujua ukweli, Shukrani kwa CAG, TAKUKURU kwa uchunguzi. Pia nawashukuru PAC, jana tulitulia kuwasikiliza PAC na leo tutulie tusikilize utetezi wangu.
Spika wa Bunge, Anne Makinda.
 Miaka ya 1990 tulikuwa tuna upungufu wa umeme kutokana na maji, 1994 serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa inamilikiwa na VIP ya Tanzania iliyokuwa na 30% na Mechmar ya Malaysia 70%.
 Kulingana na mkataba, majukumu ya IPTL yalikuwa kujenga, kumiliki na kuendesha hivyo utaifishaji utaiingiza serikali katika matatizo makubwa ikiwemo kushtakiwa kimataifa pia itafukuza wawekezaji binafsi. TANESCO na IPTL walisainiana mkataba wa miaka 20, hata hivyo uzalishaji haukuanza mara moja kutokana na mgogoro ulioibuka baina ya TANESCO na IPTL


IPTL ilianza kuzalisha umeme 2002 hivyo mkataba ukaanza kuhesabiwa hapo, kutokana na mgogoro ikafunguliwa Escrow Account na Escrow ilizungumziwa toka mkataba wa 1995.

2004 TANESCO ilifungua shauri kupinga tozo la capacity charge

Taarifa hii sio ya kweli kwani TANESCO haijawahi kufungua kesi yoyote dhidi ya Standard Charted kama ilivyosemwa na PAC. Kesi hiyo ilifunguliwa na Standard Charted na ilikuwa haihusu capacity charge. Hamna kokote mkataba kati ya Standard Charted na TANESCO.

Makinda ameingilia na kusema ripoti itatolewa baada ya wabunge kudai ripoti hiyo.

Muhongo anaendelea

Uwiano wa mtaji ni 70 kwa 30, na uamuzi haujabadilishwa na mahakama yoyote. 2004 kampuni ya Mkono and CO Advocates iliishauri TANESCO iendelee kupinga capacity charge London. Hata hivyo, haikuishauri TANESCO kufungua kesi za TANZANIA wala mahakama ya kimataifa. Hadi 2013 Jaji Utamwa anatoa hukumu ya mgogoro wa wanahisa wa IPTL kulikuwa hamna kesi yoyote kuhusu tozo ya IPTL.

UUZAJI WA HISA ZA VIP
Kutokana na kutokubaliana Mechmar iliishauri VIP ifungue shauri. VIP ilifungua shauri Tanzania ikiomba IPTL ifilisiwe. Uamuzi ulitolewa kwa shauri la VIP. Chini ya Kimario, alpewa mfilisi wa muda kulinda mali za IPTL, kufanya uchunguzi ili mahakama iweze kutoa uamuzi. Uamuzi ulitoka IPTL iweke kwenye ufilisi kamili chini ya RITA. Hukumu ilipingwa mahakama ya rufaa ikianisha dosari katika uamuzi wa mahakama kuu na Standard Charted Hong Kong. Mahakama ya rufaa ilikubaliana na hoja hiyo na ilipelekwa tena kwa mfilisi wa muda kukusanya madeni, kusuluhisha mogogoro na kuendesha mitambo ya IPTL kwa niaba ya IPTL.

Serikali haiwajibiki kuingilia hisa za makampuni binafsi, mauzo ya hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu endapo yatatambuliwa na BRELA. Uhamishaji wa hisa 7 ulisajiliwa hapa nchini. Kamati katika uthibitisho huo inakubali hisa za Mechmarr unamilikiwa na PAP.

Hisa saba za IPTL zinatambuliwa pia na Standard Charted, Kama PAP haimiliki asilimia sabini kwa nini wana makubaliano na Standard Charted ya Uingereza?

Ilifilisiwa Malaysia na sio Tanzania, madai ya Standard Charted dhidi ya TANESCO ni kwa sababu IPTL waliweka dhamana mtambo wa kuzalishia umeme, Lakini benki ya Hong Kong ilikosa sifa ya kufungua shauri Tanzania hivyo ilifungulia Uingereza.

VIP chini ya usuluhishi wa RITA iliuza hisa zake PAP kwa dola milioni 70 na ndivyo ilivyomaliza mgogoro wa IPTL. Mimi sio dalali wa hii biashara bali ni dalali wa (anasema mambo mazuri aliyoyafanya)
Makinda amekuwa mkali kidogo kwa Muhongo asome taarifa na asiseme ambayo hayamo.

AKAUNTI YA ESCROW
TANESCO kwa ushauri wa Mkono walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme na makadirio ya mtaji walitoa notisi (Invoice disputes notice) ya kupinga usahihi wa malipo. Alietoa ushauri ni kampuni ya Mkono, 2006 serikali ulisaini mkataba wa kufungua Akaunti ya Escrow.

MMILIKI WA FEDHA YA ESCROW
Akaunti ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa na TANESCO. PAC walitoa mapendekezo kuwa imethibitisha kuwa mchakato wa kutoa pesa Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kutakatishwa na benki mbili

TAHADHARI ZILIZOCHUKULIWA
Serikali ilichukua kinga kutoka IPTL, kwa mujibu wa kinga IPTL itawajibika yakitokea madai yoyote na ilipitiwa na mwanasheria mkuu wa serikali. (Yoyote anaedai chochote aende IPTL)

PAC wameeleza serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha juu ya madai mapya kama yangejitokeza kitu ambacho sio kweli.

DHANA YA MADAI YA BILIONI 321
Madai kwamba IPTL inaidai 321 Bilioni, bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG hakionyeshi madai haya.

Madai yaliyowasilishwa na mufilisi, yalitakiwa kuhakikiwa lakini hayakuhakikiwa na hayakuwa na uhalali wowote.

Kamati ya PAC, wamesema yana uhalali japo uhalali wake unategemea maamuzi.

MADENI TANESCO
Wazri Muhongo amesema Tanesco haijaanza kutengeneza pesa kwa manufaa ya Umma ina madeni. Hivyo hamna fedha za umma popote kuna madeni tu.

MWANASHERIA WA TANESCO

Prof. Muhongo amesema Mwanasheria wa Tanesco anayedaiwa kufukuzwa kazi taarifa hiyo si ya kweli na bwana huyo amedanganya umma.
Ukweli ni kwamba Mwanasheria huyo alileta ombi la kusafiri kwenda Malaysia kwa kumdanganya mwajiri wake kwa kuandika barua kuwa anakwenda na Mwanasheria Mwandamizi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Hivyo hakufukuzwa kazi bali aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa kumwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco mwezi Februari mwaka huu#TegetaEscrow

BUNGE LAAHIRISHWA

Spika wa Bunge, Anne Makinda ameahirisha kikao cha bunge mpaka jioni saa 11 baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo kumaliza kutoa utetezi wa serikali.

No comments:

Post a Comment