Spika wa Bunge, Anne Makinda.
IPTL ilianza kuzalisha umeme 2002 hivyo mkataba ukaanza
kuhesabiwa hapo, kutokana na mgogoro ikafunguliwa Escrow Account na Escrow
ilizungumziwa toka mkataba wa 1995.
2004 TANESCO ilifungua shauri kupinga tozo la capacity
charge
Taarifa hii sio ya kweli kwani TANESCO haijawahi kufungua
kesi yoyote dhidi ya Standard Charted kama ilivyosemwa na PAC. Kesi hiyo
ilifunguliwa na Standard Charted na ilikuwa haihusu capacity charge. Hamna
kokote mkataba kati ya Standard Charted na TANESCO.
Makinda ameingilia na kusema ripoti itatolewa baada ya
wabunge kudai ripoti hiyo.
Muhongo anaendelea
Uwiano wa mtaji ni 70 kwa 30, na uamuzi haujabadilishwa na
mahakama yoyote. 2004 kampuni ya Mkono and CO Advocates iliishauri TANESCO
iendelee kupinga capacity charge London. Hata hivyo, haikuishauri TANESCO
kufungua kesi za TANZANIA wala mahakama ya kimataifa. Hadi 2013 Jaji Utamwa
anatoa hukumu ya mgogoro wa wanahisa wa IPTL kulikuwa hamna kesi yoyote kuhusu
tozo ya IPTL.
UUZAJI WA HISA ZA VIP
Kutokana na kutokubaliana Mechmar iliishauri VIP ifungue
shauri. VIP ilifungua shauri Tanzania ikiomba IPTL ifilisiwe. Uamuzi ulitolewa
kwa shauri la VIP. Chini ya Kimario, alpewa mfilisi wa muda kulinda mali za
IPTL, kufanya uchunguzi ili mahakama iweze kutoa uamuzi. Uamuzi ulitoka IPTL
iweke kwenye ufilisi kamili chini ya RITA. Hukumu ilipingwa mahakama ya rufaa
ikianisha dosari katika uamuzi wa mahakama kuu na Standard Charted Hong Kong.
Mahakama ya rufaa ilikubaliana na hoja hiyo na ilipelekwa tena kwa mfilisi wa
muda kukusanya madeni, kusuluhisha mogogoro na kuendesha mitambo ya IPTL kwa
niaba ya IPTL.
Serikali haiwajibiki kuingilia hisa za makampuni binafsi,
mauzo ya hisa yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu endapo yatatambuliwa
na BRELA. Uhamishaji wa hisa 7 ulisajiliwa hapa nchini. Kamati katika
uthibitisho huo inakubali hisa za Mechmarr unamilikiwa na PAP.
Hisa saba za IPTL zinatambuliwa pia na Standard Charted,
Kama PAP haimiliki asilimia sabini kwa nini wana makubaliano na Standard
Charted ya Uingereza?
Ilifilisiwa Malaysia na sio Tanzania, madai ya Standard
Charted dhidi ya TANESCO ni kwa sababu IPTL waliweka dhamana mtambo wa
kuzalishia umeme, Lakini benki ya Hong Kong ilikosa sifa ya kufungua shauri
Tanzania hivyo ilifungulia Uingereza.
VIP chini ya usuluhishi wa RITA iliuza hisa zake PAP kwa
dola milioni 70 na ndivyo ilivyomaliza mgogoro wa IPTL. Mimi sio dalali wa hii
biashara bali ni dalali wa (anasema mambo mazuri aliyoyafanya)
Makinda amekuwa mkali kidogo kwa Muhongo asome taarifa na
asiseme ambayo hayamo.
AKAUNTI YA ESCROW
TANESCO kwa ushauri wa Mkono walitoa hoja kuwa gharama za kununua
umeme na makadirio ya mtaji walitoa notisi (Invoice disputes notice) ya kupinga
usahihi wa malipo. Alietoa ushauri ni kampuni ya Mkono, 2006 serikali ulisaini
mkataba wa kufungua Akaunti ya Escrow.
MMILIKI WA FEDHA YA ESCROW
Akaunti ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa
na TANESCO. PAC walitoa mapendekezo kuwa imethibitisha kuwa mchakato wa kutoa
pesa Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kutakatishwa na benki mbili
TAHADHARI ZILIZOCHUKULIWA
Serikali ilichukua kinga kutoka IPTL, kwa mujibu wa kinga
IPTL itawajibika yakitokea madai yoyote na ilipitiwa na mwanasheria mkuu wa
serikali. (Yoyote anaedai chochote aende IPTL)
PAC wameeleza serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha juu
ya madai mapya kama yangejitokeza kitu ambacho sio kweli.
DHANA YA MADAI YA BILIONI 321
Madai kwamba IPTL inaidai 321 Bilioni, bodi ya TANESCO
imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG
hakionyeshi madai haya.
Madai yaliyowasilishwa na mufilisi, yalitakiwa kuhakikiwa
lakini hayakuhakikiwa na hayakuwa na uhalali wowote.
Kamati ya PAC, wamesema yana uhalali japo uhalali wake
unategemea maamuzi.
MADENI TANESCO
Wazri Muhongo amesema Tanesco haijaanza kutengeneza pesa kwa
manufaa ya Umma ina madeni. Hivyo hamna fedha za umma popote kuna madeni tu.
MWANASHERIA WA TANESCO
Prof. Muhongo amesema Mwanasheria wa Tanesco anayedaiwa
kufukuzwa kazi taarifa hiyo si ya kweli na bwana huyo amedanganya umma.
Ukweli ni kwamba Mwanasheria huyo alileta ombi la kusafiri
kwenda Malaysia kwa kumdanganya mwajiri wake kwa kuandika barua kuwa anakwenda
na Mwanasheria Mwandamizi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
Hivyo hakufukuzwa kazi bali aliomba kuacha kazi mwenyewe kwa
kumwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco mwezi Februari mwaka
huu#TegetaEscrow
BUNGE LAAHIRISHWA
Spika wa Bunge, Anne Makinda ameahirisha kikao cha bunge
mpaka jioni saa 11 baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo kumaliza
kutoa utetezi wa serikali.
No comments:
Post a Comment