Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kilwa Masoko katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Mkapa Square mjini Kilwa wakati wa ziara yake ya ya mikoa ya Lindi na mtwara itakayochukua siku 16 akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi na kuhimiza uhai wa chama, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anaongozana na Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi .(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KILWA MASOKO-LINDI)Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi wa Kilwa Masoko katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mkapa Square .
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Nyerere Square..Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali walikokuwa wakihutubia.
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungala Maarufu kama Bwege akiwa na wanachama wenzake wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Kilwa Masoko leo.
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungala Maarufu kama Bwege akifurahia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Kilwa Masoko leo.
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali walikokuwa wakihutubia.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega akimpongeza Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndugu Abdalah Ulega akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Kikundi cha muziki kikitumbuiza katika mkutano huo.
Wananchi wakiserebuka na muziki katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha mtambo wa kutengeneza barabara wakati akishiriki katika ujenzi wa mmradi wa barabara ya Kwa Mkocho inayoelekea Kilwa Kivinje wilayani Kilwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda kwenye Mtambo wa kutengeneza barabara tayari kwa kushiriki ujenzi wa barabara hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega wakati alipokuwa akiendesha mtambo wa kutengeneza barabara aliposhiriki katika ujenzi wa mradi wa barabara ya Kwa Mkocho inayoelekea Kilwa Kivinje.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye mtambo wa kutengeneza barabara ya Kwa Mkocho mara baada ya kushiriki ujenzi huo, kushoto anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya chanzo cha maji wakati alipokagua shamba la kilimo cha uwagiliaji Mavuji kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua chanzo cha maji wakati alitembelea kilimo cha Umwagiliaji kata ya Mavuji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa shamba la umwagiliaji kata ya Mavuji.
Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda akisalimia wananchi Nangurukuru.
Mbunge wa jimbo la Mtama, Mlezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kilwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa Mh Bernard Membe akisalimia wananchi Nangurukuru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu ABdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kabla ya kushiriki ujenzi wa nyumba ya daktari katika zahanati ya Nangurukuru
Mradi wa shambi la kuvuna chumvi Miima wilayani Kilwa
Baadhi ya wananchi wakisafisha chumvi katika mradi wa kuvuna chumvi Miima Kilwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za uvunaji wa Chumvu katika shamba la Miina wilayani Kilwa.
No comments:
Post a Comment