Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Neawala Mh George Mkuchika mara baada ya kuwasili mjini Newala akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mtwara ziara yenye lengo la kukagua na kuhimiza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu Mkuu Kinana emeembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa miondombinu ya maji , Zahanati Ofisi za Chama cha Mapinduzi na kuzungumza na wananchi katika mikutano mbalimbali, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE -NEWALA-MTWARA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana viongozi wa kiwanda cha kubangua korosho mjini Newala kulia Niry Patel Mratibu wa Usafirishaji na katikati ni Ednyadayu Meneja wa ufundi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubangua korosho na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi ya kubangua korosho
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mhandisi wa Maji Newala Bw. Nsajigwa Said wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Malatu mjini Neawala.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa maji katika kata ya Malatu kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mtwara B. Halima Dendegu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo katika ujenzi wa tanki la maji la kijiji cha Kilidu kwa pamoja na wafanyakazi wa katika mradi huo wa tatu kutoka kulia aliyesimama ni Mbunge wa jimbo la Neawala Mh. George Mkuchika.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dr Yudas Ndugile Mganga mkuu wa wilaya ya Newala wakati alipokagua jengo jipya la Kituo cha Afya Mkwedu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa wilaya ya Newala BwMarx Simon Kamaoni na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishuhudia aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda Sijaona akivua shati la CHADEMA na kuvaa la CCM mara baada ya kuondoka katika chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitupa shati hilo
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda akiwa amekabidhi kadi yake na ya mke wake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kujiunga na CCM mjini Newala kulia ni Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakisisitiza jambo katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakikabidhi pikipiki kwa vijana ambazo zimekopeshwa kwao ili kujikomboa kiuchumi.
Umati wa watu wakisikiliza mkutano huo.
No comments:
Post a Comment