Kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kwa kile walichomtuhumu kuiba simu katika moja ya duka lililopoa maeneo ya Makumbusho karibu na Kituo cha Daladala, jijini Dar es Salaam.
Wakielezea tukio hilo mashuhuda walisema kuwa kijana huyo aliingia katika duka hilo lililokuwa na mwanadada na kupora simu iliyokuwa juu ya kabati la bidhaa na kutimka nayo jambo lililomfanya mwanadada huyo kutoka nje na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada.
Kama ilivyo kawaida kijana huyo aliungaishiwa na kila mtu aliyemuana akitimka na kufanikiwa kumtia nguvuni na kuanza kula kichapo hadi aliporejesha simu ya mdada huyo. Baadaye aliachiwa huru na kuondoka zake.
Kjana huyo akijibu maswali baada ya kichapo
No comments:
Post a Comment