Pages

Monday, November 17, 2014

PICHA::HII NI KUHUSU VIONGOZI WA UKAWA WALIOHAMIA ACT


 Na Karoli Vinsent

        CHAMA kipya cha Siasa nchini cha Tanzania Tanzania Alliance for change and Transparency ACT kimezidi kuvuna wanachama wapya kutoka vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya wananchi UKAWA vyama hivyo ni Chadema,CUF na NCCR- mageuzi ,baada ya Viongozi mbalimbali kutoka vyama hivyo kuhamia kwenye chama hicho.

       Wanachama hao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF mkoa wa Ilala,Ramadhan Khamis na aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jimbo la Korogwe na Afisa Habari Taifa wa chama hicho Tony Kamkanda

Viongozi mbambali kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakihamia Chama cha ACT Wakipokolewa na Katibu Mkuu wa Chama ACT-Samsoni Mwigamba kulia

 Akithibitisha kuwapokea wananchama hao  Jijini Dar es Salaam ,Katibu mkuu wa Chama  cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba wakati wa Mkutano na Waandishi ambapo Mwigamba amesema  huu sio mwisho kwani chama hicho kwanzia sasa kitapokea wanachama wengi tena viongozi wakubwa tu kutoka vyama vingine vya siasa na akasema


 chama hicho kinawakalibisha wanachama wote kutoka vyama vyote vya siasa nchini kuhamia kwenye chama hicho kupata  Demokrasia ya kweli na yenye kulijenga Taifa kimaendeleo.



          “Nawakalibisha sana wanachama wengine kuiga mfano wa wananchama hawa wapya kwani ACT ni chama ambacho chenye nia ya dhati ya kuendeleza Demkokrasia ,na sisi tuko na tofauti na vyama vingine vya upinzani  ambavyo badala ya kujenga chama vimekuwa vikiishia kuzungumza wahasisi na chama chetu hakina nia hiyo bali kiko kwa ajiri na kumkomboa mtanzania wa leo”Alisema Mwigamba



         Kwa upande wake wanachama hao waliohamia ACT –Tanzania walisema wamehamia chama hicho baada ya kuchoshwa na mifumo isiyokuwa na tifa na yenye kuua Domkrasia nchini kwenye Vyama hivyo ambavyo wanadai viko kwa ajiri ya kutafuta pesa na sio kumkomboa mtanzania wa leo mwenye matatizo lukuki.

      

           Katika Hatuo Nyingine Chama Kipya cha Siasa nchini kinatarajiwa kuzinduliwa Rasmi tarehe 5,desemba mwaka huu,na kushuhudiwa na watu mbalimbali pamoja na vyama vingine vya kisiasa nchini.

       

       Akizungumzia Uzinduzi huo Katibu Mkuu huyo wa ACT-Tanzania Samson Mwigamba alisema licha ya uzinduzi huo pia chama hicho kinatarajia kumfanya mkutano wake mkuu wa Mwaka unaotarajia kufanyika Jijin Dar Es Salaam na kuwataka wananchi kukiunga chama hicho chenye malengo mazuri kwao.



          KUHUSU MWIGAMBA KUFUKUZWA ACT-TANZANIA


Mwigamba alisema hawezi kufukuzwa ACT kwani  yeye yupo hapo kisheria na wanao sema hivyo na malalamiko yapo chama hicho  kitachukua hoja zao kama mapendekezo ya kukijenga chama hicho na kusema chama hicho hakina wahasisi kama wanavyodai .

No comments:

Post a Comment