Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 23, 2014

Kikongwe wa Miaka 101 aona bahari kwa mara ya kwanza

Wiki kadhaa kabla ya kufika miaka 101, Ruby Holt ameona Bahari kwa mara ya kwanza.
Maisha yake yote amekuwa akiishi maeneo ya shambani,jimboni Tennessee akivuna pamba, hivyo amesema hakuwa na muda wala pesa za kumfikisha ukingoni mwa bahari.
Ruby anasema amesikia watu wakiongelea kuhusu bahari,uzuri wake na kuwa alitaka kuiona lakini anasema hakupata nafasi.
Hatimaye aligharamiwa kwa safari kwenda ghuba ya Mexico.


Alilipiwa gharama hizo na kituo kinacholea wazee na kutoa msaada kwa wazee hao kutimiza haja za nyoyo na ndoto walizokuwa nazo katika maisha yao.
Mkurugenzi wa Nyumba inayolea wazee ambayo bi.Holt anaishi amesema wafanyakazi wawili walijaza ombi la kikongwe huyo na kubaini kuwa alitamani kuona bahari kwa mara ya kwanza.
Bi Holt alionekana mwenye furaha isiyo ya kifani baada ya kutimiziwa haja yake kwa kuwa alisafiri mpaka Alabama kwa kuwa kwa miaka mingi aliwahi kutoka mara moja tu nje ya jimbo la Tennessee.
Bibi huyo mwenye watoto wanne, amesema alikua ametingwa mno na kazi katika shamba, au akifanya kazi katika kampuni ya kutengeneza mashati kiasi cha kushindwa kusafiri, zaidi ya hayo familia haikua na hela.

Safari ya mpaka ghuba hiyo ni umbali wa maili 400.chanzo BBC

No comments:

Post a Comment