Wiki kadhaa kabla ya kufika miaka 101, Ruby Holt ameona
Bahari kwa mara ya kwanza.
Maisha yake yote amekuwa akiishi maeneo ya shambani,jimboni
Tennessee akivuna pamba, hivyo amesema hakuwa na muda wala pesa za kumfikisha
ukingoni mwa bahari.
Ruby anasema amesikia watu wakiongelea kuhusu bahari,uzuri
wake na kuwa alitaka kuiona lakini anasema hakupata nafasi.
Hatimaye aligharamiwa kwa safari kwenda ghuba ya Mexico.
Alilipiwa gharama hizo na kituo kinacholea wazee na kutoa
msaada kwa wazee hao kutimiza haja za nyoyo na ndoto walizokuwa nazo katika
maisha yao.
Mkurugenzi wa Nyumba inayolea wazee ambayo bi.Holt anaishi
amesema wafanyakazi wawili walijaza ombi la kikongwe huyo na kubaini kuwa
alitamani kuona bahari kwa mara ya kwanza.
Bi Holt alionekana mwenye furaha isiyo ya kifani baada ya
kutimiziwa haja yake kwa kuwa alisafiri mpaka Alabama kwa kuwa kwa miaka mingi
aliwahi kutoka mara moja tu nje ya jimbo la Tennessee.
Bibi huyo mwenye watoto wanne, amesema alikua ametingwa mno
na kazi katika shamba, au akifanya kazi katika kampuni ya kutengeneza mashati
kiasi cha kushindwa kusafiri, zaidi ya hayo familia haikua na hela.
Safari ya mpaka ghuba hiyo ni umbali wa maili 400.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment