Maafisa watano wakuu wa mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori
nchini Uganda wamesimamishwa kazi kwa muda baada ya zaidi ya tani moja ya pembe
za Ndovu zilizokuwa zimenaswa kutoweka kutoka katyika kituo cha serikali.
Pembe hizo zilikuwa na thamani ya dola milioni moja.
Msemaji wa polisi Fred Enanga, amesema kuwa Pembe hizo
ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwa angalau miaka kumi, zilizpaswa kuchomwa.
Inadaiwa kuwa pembe hizo zilikuwa zitumike kama mtego kwa
wawindaji haramu wa ndovu lakini
maafisa hoa waliziuza kwa manufaa yao wenyewe.
Shirika la kimataifa la polisi, Interpol lilikuwa limetakiwa
kusidia Uganda katika kuchunguza wizi huo, kufuatia wito kutoka kwa Rais kutaka
wahalifu hao kuwakamata.
Watano walioachishwa kazi ni pamoja na mlinzi mkuu wa mbuga
za kitaifa.
Maafisa wakuu walisema kuwa kama kawaida waliangalia kuona
iwapoa pembe hizo zilizokuwa na uzito wa kilo 1,335 zipo katika sehemu ambako
huhifadhiwa kila siku, ingawa hawakuzipata dalili ya kwamba pembe hizo zilikuwa
zimeibiwa.
Wachunguzi wanashuku kuwa wafanyakazi wa serikali wamekua
wakishirikiana na walanguzi kuhusu ambavyo wangezisafirisha pembe hizo
Inadaiwa baadhi ya maafisa wafisadi walikuwa wamesema
wanazihifadhi Pembe hizo ili waweze kuzitumia kama mtego kwa wawindaji haramu
lakini baadaye wao ndio waliofaidika kwa kuziuza.
Visa vya uwindaji haramu, vimeongezeka kote barani Afrika
katika miaka ya hivi karibuni vikichochewa na biashara ya pembe hizo barani
Asia hasa pembe za vifaru ambazo zinadaiwa kuwa tiba ya kienyeji.chanzo Bbc
No comments:
Post a Comment