Pages

Thursday, November 6, 2014

LIST YA WANAMUZIKI WA KIKE WANAOLIPWA ZAIDI HII HAPA,BEYONCE AONGOZA

BEYONCE 'ATESA' KWA KIPATO
Akiingiza zaidi ya dola milioni 115, Beyonce amekuwa mwanamke anayelipwa zaidi katika muziki mwaka huu. Alikuwa na "mwaka wenye mafanikio zaidi", akifanya maonesho 95 na kuingiza wastani wa dola milioni 2.4 katika kila jiji, kwa mujibu wa Forbes. Mikataba na makampuni kama vile Pepsi na H&M, pamoja album iliyotolewa 'ghafla' Disemba 2013, 


zimemsaidia kushika nafasi hiyo. Albam hiyo ilitolewa kwenye iTunes bila hata kufanyiwa matangazo ya utambulisho. Beyonce ametangaza pia kuwa atatoa album baadaye mwezi ujao, itakayokuwa na nyimbo mpya na video ya tamasha.
Taylor Swift ameshika nafasi ya pili katika orodha hiyo ya Forbes, akiingiza takriban dola milioni 64. Nafasi ya tatu imechukuliwa na Pink, aliyefanya matamasha 85 katika kipindi ambacho Forbes ilikuwa ikifanya tathmini yake. Alikadiriwa kuingiza dola milioni 52. Wasanii wengine katika orodha hiyo ni Rihanna katika nafasi ya nne akiingiza dola milioni 48 na Katy Perry katika nafasi ya tano aliyetengeneza dola milioni 40. Forbes ilipiga hesabu zake kwa kutazama mapato kutokana na "matamasha, mauzo ya rekodi, mauzo ya bidhaa za kimuziki, mikataba ya makampuni ya kibiashara na mengineyo" kati ya Juni 2013 na Juni 2014. Baadhi ya wasanii maarufu ambao walikosa nafasi za juu ni pamoja na Madonna, Nicki Minaj na Alicia Keys.
Orodha ya kumi bora:
1: Beyonce - Dola 115m
2: Taylor Swift - Dola 64m
3: Pink - Dola 52m
4: Rihanna - Dola 48m
5: Katy Perry - Dola 40m
6: Jennifer Lopez - Dola 37m
7: Miley Cyrus - Dola 36m
7: Celine Dion - Dola 36m
9: Lady Gaga - Dola 33m
10: Britney Spears - Dola 20m

Chanzo: Forbes/BBC

No comments:

Post a Comment