Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb) akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Bunge leo na kuainisha hatua madhubuti za kuchukuliwa na serikali ili kukomesha mauaji baina ya wakulima na wafugaji yanayoendelea Mkoani Manyara wilaya Kiteto na sehemu nyingine nchini.
Wajumba wa Kamati ya Uongozi ya Bunge wakimsikiliza Waziri Mkuu kwa umakini mkubwa alipokuwa akitanabaisha jinsi Serikali isivyopendezwa na mauaji ya Kiteto na jinsi ilivyojipanga kukomesha kabisa mauji hayo.
Naibu Spika na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwa jinsi walivyozungumza na Mhe, Waziri Mkuu kwa moyo wa kizalendo kwa nchi yao.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) akitoa ushauri kwenye Kamati ya Uongozi jinsi ya kuwasilishwa Bungeni taarifa za Tume mbalimbali leo. Picha na Prosper Minja-Bunge
No comments:
Post a Comment