Zambia inafanya mazishi ya kitaifa ya Rais Michael Sata
ambaye alifariki dunia mwezi uliopita katika hospitali moja nchini Uingereza
akiwa na umri wa miaka 77. Maelfu ya watu wamehudhuria misa maalum iliyofanyika
kwenye uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka. Viongozi mbalimbali wa kimataifa ni
miongoni mwa waliohudhuria. Akijulikana kama "King Cobra" kutokana na
matamshi makali, Rais Sata alichaguliwa kuwa rais mwaka 2011. Nchi hiyo kwa
sasa inaendeshwa na kaimu rais, na uchaguzi utafanyika mwezi Januari.
HARAMBEE YA MWEZESHE ATEMBEE YAKUSANYA BILIONI 1
-
GSM Foundation kwa kushirikiana na Hospitali ya CCBRT na klabu ya Yanga
waliendesha Harambee ya Mwezeshe atembee kwa ajili ya kukusanya fedha ili
kutibu ...
7 hours ago
No comments:
Post a Comment