Kwa kimya kingi, mtoto Neelofar mwenye umri wa miaka mitatu
pekee amepakatwa na nyanyake katika kiti cha nyuma cha texi ikimkimbiza
hospitalini.
Ndani ya mwili wake kuna kijipaipu ambacho amewekewa
kutumiwa kumpa dawa kama huduma ya kwanza kabla ya kufikishwa hospitalini.
Mkono wake mmoja umefungwa kwa bandeji ambako kuna kifaa
kinachotumiwa kuingizia maji mwilini mwake.
Mtoto Neelofar yuko hali mahututi, baada ya kubakwa na
anahitaji matibabu maalum ambayo anaweza kupokea tu hospitalini.
Siku chache zilizopita, Neelofar alikuwa anacheza na rafiki
zake nje ya nyumba yao wakati mwanamume mmoja alimteka na kwenda naye katika
shamba lililokuwa karibu na nyumba hiyo.
Kulingana na familia yake na wahudumu wa afya, mbakaji
alimfunga kinywa mtoto huyo na kumbaka na hata kujaribu kumuua.
Kwa karibu mtoto huyo ana majeraha mabaya na pia anahisi
uchungu mwingi wakati akiendelea kupokea matibabu hospitalini.
Mwanamume huyo alimziba pua na mdomo mtoto kujaribu
kumkosesha pumzi mtoto kwa sababu aliogopa kwamba angepiga mayowe. Mtoto huyo
alikuwa ana alama nyingi shingoni mwake dalili ya majereha aliyoyapata.
Wazazi wa mtoto huyo hawakuwa nyumbani wakati wa kitendo
hicho cha unyama.
Kwa bahati nzuri, familia ya mtoto inasema kuwa mwanamume
aliyekuwa anapita karibu na nyumba hiyo ndiye alisikia mayowe yake na kumuokoa.
Neelofar alipatikana akivuja damu na akiwa ametupwa karibu
na msikiti katika kijiji hicho.
Polisi wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 18 kuhusiana
na unyama huo.
Inaarifiwa kuwa mwanamume huyo ni jirani na mtu
anayejulikana kwa familia ya mtoto huyo.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment