MIMBA inayotungia nje ya mfuko wa uzazi kwa kitaalamu inafahamika
kama ectopic pregnancy. Hii mimba inayotungia nje ya mfuko wa kizazi
huwa inakaa ndani ya mirija ya uzazi. Mimba kama hii huwa anaipatapa
mwanamke kwa njia ya kawaida au anaweza kuipata kwa njia ya
upandikizaji.
Mimba hii inaweza kutoa ndani ya mirija ya uzazi ila wataalamu wanasema
kwamba zaidi ya asilimia 97 huwa inatokea kwenye mirija ya uzazi.
Sababu
Uharibifu wa mirija ya uzazi
Mara nyingi uharibifu wa mirija ya uzazi kwa njia yoyote ile ndio
huwa inapelekea kutokea kwa utungaji wa mimba nje ya mfuko wa uzazi
ambayo hujiotesha katika mirija ya uzazi na hatima yake huleta shida na
matatizo makubwa.
Kwanza ieleweke mwanamke anaweza kupata mimba hii bila sababu yoyote na
si kila mwanamke ambaye anapata ectopic pregnancy aliwahi kuwa na
kisababishi fulani.
Lakini wanawake wengi wanapata hizi mimba kutokana na sababu nyingi
mbalimbali. Mara nyingi mwanamke ambaye alishawahi kupata mimba ambayo
imetunga nje ya mfuko wa uzazi ana hatari tena ya kupata tatizo hili.
Kujaa maji kwa mirija ya uzazi
Tatizo la kujaa maji kwa mirija ya uzazi linaweza kusababisha mimba
kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Kama mrija mmoja wa mwanamke utakuwa na
maji ukazuia yai moja kupita na mimba ikatunga pale pale hata kama
mrija huo utakatwa maambukizi yatakuwa yashahamia katika mrija wa
upande wa pili. Kwa hiyo mwanamke ana hatari ya kupata tena mimba
itakayotunga nje ya mfuko wa uzazi.
Kutokea kwa vimbe mbalimbali katika mfuko wa kizazi
Kuna viti vingi ambavyo huweza kusababisha tatizo hili ikiwemo pia
kutokea kwa vimbe katika mirija ya uzazi nazo huweza kusababisha mimba
kutunga nje ya mfuko wa uzazi.
Maambukizi ya magonjwa ya ngono
Tatizo jingine ambalo linaweza kusababisha mimba kutunga nje ya
mfuko wa uzazi ni maambukizi ya magojwa ya ngono kama gonorea na
magonjwa ya zinaa.
Hivyo mwanamke ambaye ameugua magonjwa haya huko nyuma ana hatari kubwa
ya kupata ectopic pregnancy kwa sababu madaktari wanasema kitendo cha
kuugua magojwa ya ngono kinamsababishia wanamke kupata tatizo la PID.
Lakini si magojwa ya ngono pekee hata yale ambayo hayaambukizwi. Wako
bacteria mbalimbali ambao mwanamke anaweza kuwapata kupitia njia
mbalimbali nao wanaweza kufanya tatizo hili.
Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi
Kwa kawaida mimba ambayo inatungia nje ya uzazi muda mwingi huwa
haionyeshi dalili hadi pale zinapokaribia wiki sita au nane baada ya
mwanamke kuona hedhi yake ya mwisho.
Kwa ukubwa wa mimba ile inaweza kuwa tayari ikawa imeshazidi uwezo wa
kuhimili uwezo wa mirija ya uzazi na hivyo kumfanya mwanamke kupata
maumivu makali tumboni chini ya kitovu.
Kuona siku wakati ni mjamzito
Dalili nyingine ni mwanamke kupata matone ya damu wakati mwanamke ni mjamzito.
Hii ni moja ya dalili lakini dalili nyingine ambayo ni mbaya zaidi ni
pale mwanamke ambapo anakuwa na mimba ambayo imetungia nje ya mfuko wa
uzazi na ikaendelea kukua hufikia wakati ikapelekea kupasuka kwa mirija
ya uzazi na kusababisha mshipa mkubwa wa damu ambao ni Ateri kupasuka
na hatimaye kumwaga damu nyingi tumboni.
Maumivu haya huweza kuwa makali na yanayokata kama kisu. Yanaweza kuwa
upande mmoja zaidi wa nyonga ingawa si lazima yawe upande ulio na
mimba. Na muda mwingine mwanamke hupoteza fahamu.
Matibabu
Matibabu ya mimba iliyotunga nje ya kizazi yanaweza kuwa ya aina
mbili. Aina ya kwanza ni kwa njia ya upasuaji na aina ya pili ni kwa
kutumia dawa mbadala kama za kituo cha Foreplan Clinic. Kwa matibabu
tutembelee kituoni kwetu au tembelea website www.foreplan.org.
NMB YATOA PONGEZI KWA JESHI LA POLISI MKOA WA SONGWE
-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Augustino Ignace Senga akipokea zawadi mbalimbali za ofisi ikiwa ni
pamoja...
1 hour ago
Mm imenitokea na nikafanyiwa upasuaji ila kabla yahapo nilishawah kubeba ujauzito ukaharibka kawaida je hyo inasababishwa na nn nabaada ya upasuaj je nivema kutumia njia yoyote ya uzaz wa mpango ili kujiepusha na mimba nyngne hv karbun mpk hcho kipind cha mwaka
ReplyDeleteMke wangu amepima amekutana na iyo Hali na mimba Ina miezi 4 je mtoto anatoka
ReplyDelete