Buka mdogo
|
Polisi nchini Ufaransa,askari wa zima moto na polisi
waliopewa mafunzo maalum ya kikosi cha mbwa wako katika msako mkubwa wa
kumtafuta paka mkubwa aliyeingia mjini.
Paka huyo mkubwa anaaminika kuwa ni chui mkubwa mwenye
mistari kama ya pundamilia maarufu kama buka,alionekana katika moja ya maduka
makubwa na hata kwenye maegesho ya magari mjini Paris.
Chopa inaongezea nguvu katika harakati za kumsaka buka huyo
ndani na nje ya mji wa Montevrain.Polisi wamewataka raia wa mji huo na mingine
miwili wasitoke nje ya nyumba zao ama matembezi ya jioni wakati wa zoezi la
kumsaka Buka huyo.
Wazazi wamesha chukua watoto wao mashuleni kwa magari baada
ya taarifa za kuonekana Buka huyo mjini bustanini.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment