Tumezoea Wabunge wetu wakipewa nafasi ya kuchangia jambo
ndani ya kikao cha Bunge huwa wanaanza kwa pongezi, utasikia hivi; “.. Kwanza
nimpongeze Mheshimiwa Mbunge au Waziri………”
Jumatatu kikao cha Bunge kitaendelea na nadhani hautoshtuka
ikitokea Mbunge hata mmoja akisema hivi; “… Nimpongeze sana Mheshimiwa David
Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kufunga ndoa siku ya Jumamosi..”
Yes.. Ni kweli.. Mbunge huyo amefunga ndoa leo Kigoma,
ujumbe alioandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu hapa;
“..Bwana Harusi David Kafulila akiwa na msimamizi wa ndoa yake Deo Filikunjombe
na marafiki zake David Silinde na Mwami..” halafu kuna picha aliyoiweka akiwa
na Wabunge hao.
Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
Mhe David Kafulila akiwa kanisani na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe Zitto Kabwe na Mhe David Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma
No comments:
Post a Comment