ACHANA na mazingira ya kifo cha Bilionea maarufu wa Bukoba,
Leonard Mtensa aliyefariki saa chache baada ya kufanya mapenzi ndani ya gari
kuacha gumzo, gumzo lingine lilitokea wakati wa mazishi yake ambayo
yalihudhuriwa na wananchi wengi kutoka ndani na nje ya mkoa, mkanda kamili huu
hapa.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mazishi hayo mwanzo
mwisho, msiba huo ulikuwa wa pekee kwani haijawahi kutokea kwa yeyote kuzikwa
na umati mkubwa kiasi hicho na kusababisha watu wote wasimame kiasi cha
kuwafanya askari wa usalama barabarani kufanya kazi ya ziada kuhakikisha mambo
yanakwenda sawa.
Wananchi wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita.
“Msafara ulianzia mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika klabu yake ya
Lina’s kisha ukapitia mtaa wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba kisha kuelekea
kijiji cha Kyaikailabwa.
“Ilikuwa si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi
kutokea msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani,
trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo.
Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati
magari mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye
foleni nyumbani.
Jeneza likibebwa kuelekea makabulini.
Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka
nyumbani kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho
kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari yalijipanga
kuanzia mjini hadi kaburini.
No comments:
Post a Comment