Na Karoli Vinsent
CHAMA kipya cha Siasa nchini cha Tanzania Tanzania Alliance for change and Transparency ACT kimezidi
kuvuna wanachama wapya kutoka vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda
Umoja wa Kutetea Katiba ya wananchi UKAWA vyama hivyo ni Chadema,CUF na
NCCR- mageuzi ,baada ya Viongozi mbalimbali kutoka vyama hivyo
kuhamia kwenye chama hicho.
Wanachama
hao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF mkoa wa
Ilala,Ramadhan Khamis na aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema jimbo la Korogwe na Afisa Habari Taifa
wa chama hicho Tony Kamkanda
Viongozi mbambali kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakihamia Chama cha ACT Wakipokolewa na Katibu Mkuu wa Chama ACT-Samsoni Mwigamba kulia |
Akithibitisha
kuwapokea wananchama hao Jijini Dar es Salaam ,Katibu mkuu wa
Chama cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba wakati wa Mkutano na Waandishi
ambapo Mwigamba amesema huu sio mwisho kwani chama hicho kwanzia sasa
kitapokea wanachama wengi tena viongozi wakubwa tu kutoka vyama vingine
vya siasa na akasema
chama hicho kinawakalibisha wanachama wote kutoka vyama vyote vya siasa nchini kuhamia kwenye chama hicho kupata Demokrasia ya kweli na yenye kulijenga Taifa kimaendeleo.
chama hicho kinawakalibisha wanachama wote kutoka vyama vyote vya siasa nchini kuhamia kwenye chama hicho kupata Demokrasia ya kweli na yenye kulijenga Taifa kimaendeleo.
“Nawakalibisha sana wanachama wengine kuiga mfano wa wananchama
hawa wapya kwani ACT ni chama ambacho chenye nia ya dhati ya kuendeleza
Demkokrasia ,na sisi tuko na tofauti na vyama vingine vya
upinzani ambavyo badala ya kujenga chama vimekuwa vikiishia kuzungumza
wahasisi na chama chetu hakina nia hiyo bali kiko kwa ajiri na kumkomboa
mtanzania wa leo”Alisema Mwigamba
Kwa upande wake wanachama hao waliohamia ACT –Tanzania walisema
wamehamia chama hicho baada ya kuchoshwa na mifumo isiyokuwa na tifa na
yenye kuua Domkrasia nchini kwenye Vyama hivyo ambavyo wanadai viko kwa
ajiri ya kutafuta pesa na sio kumkomboa mtanzania wa leo mwenye matatizo
lukuki.
Katika Hatuo Nyingine Chama Kipya cha Siasa nchini
kinatarajiwa kuzinduliwa Rasmi tarehe 5,desemba mwaka huu,na kushuhudiwa
na watu mbalimbali pamoja na vyama vingine vya kisiasa nchini.
Akizungumzia Uzinduzi huo Katibu Mkuu huyo wa ACT-Tanzania Samson
Mwigamba alisema licha ya uzinduzi huo pia chama hicho kinatarajia
kumfanya mkutano wake mkuu wa Mwaka unaotarajia kufanyika Jijin Dar Es
Salaam na kuwataka wananchi kukiunga chama hicho chenye malengo mazuri
kwao.
KUHUSU MWIGAMBA KUFUKUZWA ACT-TANZANIA
Mwigamba
alisema hawezi kufukuzwa ACT kwani yeye yupo hapo kisheria na wanao
sema hivyo na malalamiko yapo chama hicho kitachukua hoja zao kama
mapendekezo ya kukijenga chama hicho na kusema chama hicho hakina
wahasisi kama wanavyodai .
No comments:
Post a Comment