Pages

Tuesday, November 18, 2014

Polisi Dar waua, wakamata majambazi

Kamishna (CP), Suleiman KovaJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewaua majambazi wawili na kuwakamata wanane katika harakati za kupambana na uhalifu wa kutumia silaha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna (CP), Suleiman Kova, alisema majambazi hao wamekamatwa katika oparesheni maalumu iliyoanza rasmi Oktoba 28 mwaka huu hadi sasa.
Kamanda Kova, aliwataja majambazi hao kuwa ni 



Ramadhani Said (37), mfanyabiashara wa mitumba mkazi wa Temeke, Rajab Ally (39), mfanyabiashara mkazi wa Mbagala, Dash John (38), mkazi wa Mbagala Chamazi na Shabani Said (28), dereva wa bodaboda mkazi wa Pugu Kajiungeni ambaye amekamatwa na silaha ya S/Gun Pump Action iliyofutwa namba yenye risasi.
Wengine ni Mohamed Mondo (32), mkazi wa Sinza Legho, Hamid Ramadhan (25), mkazi wa Mburahati, Carlos Kisitu (28), mkazi wa Mbagala Chamazi, Selemani Shabani (31), dalali wa nyumba mkazi wa Mwananyamala Kisiwani.
Aliwataja waliouwawa ni Salum Kombo (27), dereva wa bodaboda, Mkazi wa Temeke, ambaye alikuwa silaha aina ya SMG NO. 789317 pamoja na risasi 12 na Mathias Emmanuel ambaye alikutwa na bastola iliyofutwa namba ikiwa na risasi mbili ndani ya magazine.
“Jambazi huyu alikuwa anatafutwa muda mrefu kwa kujihusisha na matukio ya aina mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo tukio la kukatwa mkono askari Polisi eneo la Pugu Mnadani na kisha kupora silaha aina ya SMG,” alisema Kova
- Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment