Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya
mtu wa kutoa huduma za misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye
alikuwa anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa
Islamic State nchini Syria mwaka uliopita
Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa
mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa
Peter Kassig ameuawa.
Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao
wanasemekana kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.
Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za kubaini chimbuko la
kanda hiyo.
Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara
mwaka uliopita.
Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha
mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku
Kassig akitishiwa.
No comments:
Post a Comment