Pages

Monday, November 17, 2014

Nane wakamatwa wakitumia majina ya viongozi kutapeli

Picha na Maktaba
KUNDI  la watu nane wanaodaiwa matapeli linashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma ya kutumia majina ya viongozi wa juu wa serikali
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alisema watu hao wametiwa hatiani baada ya msako unaoendeshwa na  jeshi hilo ili kubaini genge la matapeli jijini hapa.
Mlowola, alisema kuelekea katika kipindi hiki cha 



mwisho wa mwaka kumeibuka magenge ya utapeli  wa kutumia njia za mitandao ya kijamii kitendo kinachotishia usalama wa mali za wananchi na viongozi wa serikali .
 “Hawa matapeli wanatumia majina ya viongozi wa serikali kutapeli watu mnamo octaba 3 mwaka huu walisajili laini namba 0719910914 yenye jina langu  na nyingine iliyokuwa imesajiliwa kwa jina la mlinzi wangu ambayo ni 0782091637,”alisema na kuongeza.
 “Siku ambayo walianza kuwapigia watu simu ni Octoba 4 Mwaka huu ambapo walikuwa wanawapigia huku wakiwaeleza kwamba nipo Dar es Saalam naomba msaAda wa kifedha ili nimpeleke mwanagu shuleni na siku ya pili walisema nipo Serengeti,”alisema Mlowola.
Kamanda Mlowola aliwataja waliokamatwa ni ni Googluck Kahumbwiya, Lameck Robert, Maico Ngaiza,Edson Nicolaus, Deogratius Mshikuma, Yusuph Mwanga, Hamza Hussein na Evadius Clashan ambaye ni kionozi wa kundi hilo aliyekuwa akijitambulisha kama kamanda.
Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya matapeli hao wanaotumia majina ya watu kutekeleza uhalifu wao.
Alibainisha kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment