Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika
kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi
Rafa Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina
yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo
na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika
meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda
fedha hizo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana
katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni
ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya
Nadal alivyotumia kula.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment