Saa ghali zaidi duniani imenunuliwa mnadani huko
Geneva,Uswiss kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 21.3.
Saa hiyo imetengenezwa kwa kutumia karati ishirini na moja
za dhahabu na ina uzito wa nusu kilo,saa hiyo iliyoundwa kwa mbwembwe
ilitengenezwa mahsusi kwa ajili ya mtoto wa mfanya biashara,Henry Graves mnamo
mwaka 1930.
Na ilimchukua miaka nane kwa watengeneza saa maarufu wa
Uswis kuikamilisha hiyo saa ghali ambaye ni Patek Philippe.
Saa hiyo ilinunuliwa siku mbili tu baada ya mmiliki wa
mwisho kufariki dunia kutoka falme za kiarabu Saud Bin Mohammed Al-Thani.
Mmiliki huyo alikuwa na madeni mengi ambayo yangemgharimu
nyumba yake kuuzwa na hivyo akaikabidhi saa hiyo kwenye nyumba ya mnada ya
Sothebys.
No comments:
Post a Comment