Pages

Wednesday, November 5, 2014

VENGU MUNGU AMETENDA


Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’.
Stori: Mwandishi Wetu
MUNGU mkubwa! Vengu is back from hell (Vengu amerudi toka kuzimu). Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’ ameanza kurejea katika ‘fomu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu, Risasi Jumatano linathibitisha.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa msanii huyo (jina tunalo), Vengu ambaye kwa muda mrefu alipoteza kumbukumbu kiasi cha kushindwa kuwatambua watu, sasa amejaliwa kwani anaweza kuwafahamu watu mbalimbali wanaopata nafasi ya kwenda kumjulia hali, Kigamboni jijini Dar anakoishi.
AMEANZA KUTOA ‘HI’ KWA WATU
“Bado yupo chini ya uangalizi maalum wa kifamilia, ni watu wachache wanaruhusiwa kumuona, lakini sasa hivi huwezi kuamini, watu wanaofika kumtazama anawatambua na anawapa ‘hi’.

 
TATIZO USIRI
Kutokana na usiri wa hali ya msanii huyo unaofanywa na familia yake, kumekuwa na maneno chini kwa chini ikiwa ni pamoja na uzushi wa mara kwa mara kuwa, mchekeshaji huyo maarufu, amefariki dunia na kuzikwa kwa siri jambo ambalo si la kweli.
Hata hivyo, katika namna ya kusikitisha, ndugu huyo alisema kuwa kila Vengu anapomtambua mtu anayemtembelea amekuwa akimwaga machozi hali inayoonesha kuwa anarejesha nyuma kumbukumbu zake na kugundua amekuwa mbali naye kwa muda mrefu.
Mfano wa nyumba ya Vengu.
KUREJEA KWENYE FANI
Pia ndugu huyo alisema kwa hali ya Vengu sasa anaweza kurejea kwenye kazi zake za kuchekesha kama zamani zile.“Kwa jinsi ilivyo, Vengu atarejea hivi karibuni katika kazi yake ya kuburudisha akiwa sambamba na wenzake wa Orijino Komedi kwa sababu afya yake inaimarika sana,” alisema ndugu huyo huku akikataa katakata kutoa ramani ya nyumba anayoishi Vengu ili mapaparazi wetu wende wakamjulie hali.
APEWA NYUMBA
Kana kwamba haitoshi, wakati hali yake ikisemwa na ndugu inaendelea vizuri, kuna madai kwamba msanii huyo na familia yake wamepewa nyumba ya kisasa yenye thamani ya shilingi milioni 120, sawa na wasanii wenzake akina Wakuvanga kufuatia mkataba wa kundi hilo na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
“Ni kweli afya ya Vengu kwa sasa ipo vizuri, anajitambua. Pia amepewa nyumba, kubwa tu ipo kulekule Kigamboni anakoishi lakini bado hajahamia.”
KUMBUKUMBU
Vengu alianza kuugua kidogokidogo mwaka 2009, lakini Agosti, 2011 hali yake ilikuwa mbaya, akalazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar. Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kwenda kumjulia hali.
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiaendelea kuuguzwa na familia yake huku taarifa zake zikiwa ngumu kupatikana mpaka hivi karibuni ambapo ndugu mmoja aliamua kuweka wazi hali ilivyo kwa sasa.
Ugonjwa wake mkubwa ulitajwa kushambulia sehemu ya kichwa, hasa kwenye ubongo.

No comments:

Post a Comment