Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.
WATU 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa
wamejeruhiwa baada ya basi walililkuwa wakisafiria la Kampuni ya Aljabir
kugonga treni eneo la Kiberege Ifakara Wilaya ya Kilombero.
Kamanda wa polisi
mkoani hapa Leonald Paulo alisema ajali
hiyo ilitokea jana majira ya saa 9:15 alasili baada ya basi hilo lilokuwa
likitokea Morogoro- Ifakara kugonga Treni ya Tazara iliyokuwa ikitokea Mbeya –
jijini Dar es Salaam.
Kamanda huyo alisema kati ya watu hao sita wanaume, wanne
wanawake na wawili ni watoto wakike
wenye umri kati ya miaka mitano na sita.
Kamanda Paulo aliwataja marehemu watatu waliotambulika
katika ajali hiyo kuwa ni Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62)
wakazi wa Ichonde Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Kamanda Paulo alisema
chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi
hilo lenye namba za usajili T725 ATD Scania, alivuka barabara yenye makutano na
reli bila ya kuchukua tahadhani na hivyo kuigonga treni.
Alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika
hospitali ya mtakatifu Fransis Ifakara na kituo cha afya Kibaoni kwa ajili ya
matibabu.
Kamanda Paulo alisema
miili ya marehemu nayo imehifadhiwa katika hospitali ya mtakatifu
Frances Ifakara.
Alisema dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali
hiyo kutokea na polisi wanamtafuta wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment