JUMLA
ya watoto 60 wamefanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo bure, Madaktari
Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na watakaobainika watapatiwa
matibabu.
Watoto hao ni wale ambao wazazi wao wanakipato cha chini, ambapo
mdhamini mkubwa wa matibabu hayo ni Shirika la Kimataifa Compassio
Tanzania wakishirikiana na Kanisa la Methodist.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Askofu
wa Kanisa la Methodist, Methodius Yamugu, alisema kwa kutambua umuhimu
wa watoto, wameamua kuanzisha makambi ya uchunguzi wa afya ya moyo kwa
vijana na watoto.
Yamugu alisema wameamua kuanzisha uchunguzi huo kutokana na ukweli
kwamba maradhi hayo yanaonekana kuwa changamoto kubwa hususan katika
baadhi ya familia duni.
“Utaratibu wa kuwapata watoto hawa unaanzia katika serikali za mitaa
lengo likiwa ni kuwapata watoto ambao kweli wanavigezo vinavyohitajika
na kwamba hakuna ubaguzi wa dini.
Naye kiongozi wa timu ya madaktari hao, Dk. Tatizo Wanne, alisema
matatizo ya moyo yako ya aina mbili, akibainisha kuwa kuna ya kuzaliwa
nayo ama yale anayopata mtoto baada ya kuzaliwa.
Alisema ili kuzuia mtoto asiweze kuzaliwa na matatizo hayo ni vema
wazazi wakawa makini katika kufuatilia huduma za chanjo zinazotolewa kwa
ajili ya kuzui maradhi hayo, mfano mzuri ni ile surua lubela
iliyotolewa hivi karibuni.
Alitoa wito kwa Watanzani kuwa ni lazima wakajijengea utaratibu wa
kufika kwenye vituo vya afya kwa lengo la kuchunguza afya zao pindi
watakapobainika kuwa na maradhi wapatiwe matibabu haraka.
Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Compassion, Elieshi Kisinza,
alisema ili nchi iweze kuwa na usalama katika maeneo yote, ni vema
watanzania wawekeza nguvu zao kwenye watoto.
- Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment